Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ilipanga kutekeleza jumla ya miradi mitatu ya maji. Mradi wa maji wa Kibirizi (Group scheme), Mradi wa Maji wa Kagera na mradi wa Maji wa Mgumile.
Ujenzi wa Mradi wa Kagera (Buhanda na Businde) imeshakamilika na kukabidhiwa KUWASA kwa ajili ya kuunganishwa na bomba kuu litakaloingiza maji kwenye tenki.
MRADI WA MAJI WA KAGERA
Mradi huu umegharimu Tsh 794,640,726.00. Ulianza kujengwa tarehe 01.04.2014 na kukamilika tarehe 30.01.2015. Mkandarasi alikuwa Proactive Independent Group Ltd. – Dar es Salaam chini ya Usimamizi wa UWP Consulting Ltd – Dar es Salaam. Mradi umekusudiwa kutoa huduma kwa watu 16,310 wa eneo la Kagera, Buhanda na Businde.
KAZI ZILIZOPANGWA KUFANYIKA KATIKA MRADI WA KAGERA
Kujenga chanzo cha maji na kufunga pampu 1, kujenga line ya umeme urefu wa kilometa 1 na kuweka transfoma. Kujenga tenki la ujazo wa mita 135 (Lita 135,000), Kujenga mtandao wa bomba wenye urefu wa kilometa 20.9. Kujenga magati 32 ya kuchotea maji. Kujenga nyumba ya mlinzi wa mitambo na kujenga ofisi ya mradi.
KAZI ZILIZOFANYIKA
Ujenzi wa tenki la ujazo wa mita 135 (Lita 135,000), ujenzi wa Magati ya maji (Vioski) 32 na Mtandao wa bomba wa urefu wa kilometa 17.4. Baadhi ya kazi za mradi huu zilipunguzwa kwa kuwa ulitakiwa kuunganishwa kwenye mradi mkubwa wa KUWASA.
HALI HALISI YA SASA YA MRADI
Mradi huu bado haujaanza kutoa huduma kwa sababu bado haujaunganishwa na mtandao wa maji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA) ili tenki liweze kupokea maji na kusambaza kwenye maeneo yaliyokusudiwa. Miundombinu ya mradi huu imekabidhiwa kwa KUWASA.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: kigomamcujiji@yahoo.com
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa