Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali Leo May 11, 2023 amefanya Mkutano na Wazee maarufu pamoja na viongozi wa dini wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari Mwandinga ambapo kiongozi huyo ameeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Serikali ya Awamu ya Sita
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Serikali imeendelea kuboresha Miundombinu katika kuboresha huduma za jamii na kukuza uchumi wa wakazi wa Wilaya hiyo
Amesema tayari Serikali imeleta fedha za Kitanzania kiasi cha Billion 58/= kwa ajili ya uboreshaji wa uwanja wa ndege kwa ujenzi na upanuzi wa eneo la kurushia Ndege na ujenzi wa Jengo la abiria huku akisema ujenzi wa Cherezo unaendelea kwa ajili ya ujenzi wa Meli nne (04) mpya Ziwa Tanganyika kwa gharama ya fedha za Kitanzania Billion 12/=
Amesema Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma unaendelea katika Kijiji cha Kabanga ambapo hadi sasa Halmashauri imepokea kiasi cha fedha za Kitanzania Billion 3/= kutoka Serikali kuu
Miradi mingine inayotarajiwa kujengwa ni pamoja na Ujenzi wa Shule mpya na madarasa kupitia mradi wa BOOST katika Wilaya ya Kigoma kwa fedha za Kitanzania Billion 2.7/=, ujenzi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) kwa gharama ya Bilioni 6.1/= eneo la Kamala Simbo, na ujenzi wa Hospitali ya Kanda Mkoani Kigoma
Amehitimisha kwa kusisitiza Wananchi kujishughulisha na kilimo cha Michikichi ya kisasa kutokana na Serikali kuendelea kutoa miche bure kwa Wakulima
Aidha Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi wa vyama vya Siasa, Waheshimiwa Madiwani, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na Watendaji wa Serikali
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa