Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imefunga mashine ya kuongeza virutubisho kinga katika Soko la Buzebazeba ili kuwahudumia Wananchi bure.
Aliyasema hayo Afisa lishe Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Omary Kibwana Jana Februari 02, 2026 alipokuwa akitoa elimu kwa Wananchi umuhimu kuongeza virutubisho katika chakula.
Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji imepokea mashine mbili (02)kutoka Wizara ya afya kwa ajili ya kuongeza virutubisho kinga katika vyakula na tayari Wananchi wanaendelea kunufaika kwa kuongeza virutubisho katika unga wa mahindi.
Aidha mashine nyingine inatarajiwa kufungwa Shule ya Sekondari Kigoma kwa ajili ya kuongeza virutubisho kinga katika vyakula kwa Wanafunzi.
Virutubisho vinavyoongezwa katika vyakula ni pamoja na Vitamin B, madini chuma, Zink na Asidi ya foliki yanayofaa kwa watu wote ikiwa ni katika kuongeza damu mwilini, kuepusha Kuzaliwa kwa Watoto wenye vichwa vikubwa, macho madogo, mgongo wazi, upofu , Goita na ukuaji hafifu.
Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuongeza virutubisho Kinga ambavyo ni mhimu na havibadili rangi na radha ya chakula.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa