Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa vyama vya siasa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa pamoja Leo Oktoba 18, 2024 wamefanya mkutano katika Mwalo wa Katonga ili kuhamasisha uandikishaji wa Wapiga Kura Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Viongozi wa vyama vya siasa kumi na mbili (12) wameungana kuanza kwa mikutano kuanzia sasa hadi uandikishaji utakapohitimishwa Siku ya jumapili Oktoba 20, 2024.
Vyama vya siasa vilivyoshiriki mkutano huo ni pamoja na CCM, ACT-WAZALENDO, CHAUMA, UDP, CCK, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, ADA-TADEA, UPDP na AFP.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakizungumza katika mkutano huo wa uhamasishaji, Katibu wa CCM Wilaya Kigoma Mjini, Sadick Kadulo amewataka kuendelea kujitokeza kujiandikisha ili kuhakikisha wanapata haki ya kupiga kura ili kupata viongozi bora.
Katibu wa Kigoma Mjini kutoka chama cha ACT Wazalendo, Iddi Adam amesema vyama vimeungana na Serikali kuhamasisha uandikishaji wa Wapiga Kura pasipo kujali itikadi.
Naye msimamizi wa uchaguzi Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura linawahusu Watanzania wote bila kujali Itikadi ya vyama vyao.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa